Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Waoblate wapya Wabenediktini wapokewa

Dekano wa Dekania ya Pugu, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Baltazar Minde akimvisha mmoja wa Waoblate wapya waliopokelewa, vazi la Shirika la Waoblate Wabenediktini, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya kuwapokea, iliyoadhimishwa katika Parokia ya Mtakatifu Fransisko wa Asizi – Pugu, jimboni humo. (Picha na Yohana Kasosi) Dekano wa Dekania ya Pugu, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Baltazar Minde akimvisha mmoja wa Waoblate wapya waliopokelewa, vazi la Shirika la Waoblate Wabenediktini, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya kuwapokea, iliyoadhimishwa katika Parokia ya Mtakatifu Fransisko wa Asizi – Pugu, jimboni humo. (Picha na Yohana Kasosi)

DAR ES SALAAM

Na Mwandishi wetu

Waoblate watawa wa tatu wa Shirika la Mtakatifu Benedikto, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wametakiwa kuendelea kushiriki Sala, mambo ya kiroho na kijamii katika maisha yao ya kila siku ya Utume wao.
Wito huo ulitolewa na Padri Baltazar Minde, Dekano wa Dekania ya Pugu, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakati akitoa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya kuwapokea Waoblate wapya wanane na wengine wanane kuweka Ahadi zao za Daima katika Utume huo wa Tatu, ilioadhimishwa katika Parokia ya Pugu, jijini Dar es Salaam.
“Naombeni sana katika maisha yenu haya ambayo mmeamua kujitoa wenyewe ninyi kama watu wa katika familia, basi mhakikishe mnaishi zile nia za Sala,”alisema Padri Minde.
Padri Minde alisema kuwa Waoblate waamini walio kwenye familia na kwenye ndoa ambao wameamua kujitoa maisha yao kwa ajili ya kufanya majitoleo ya sala, kazi na kujifunza zaidi mambo ya kiroho.
Alisema kuwa kila Mkristo anaweza kuomba kujiunga na Utawa huo wa Tatu katika maisha yake ili aweze kupokelewa katika Utawa huo wa Mtakatifu Benedikto.
Kwa mujibu wa Padri Minde, maana ya Waoblate ni kujitolea kwani kwa namna ya pekee ni kama sadaka ya pekee, hasa kwa wanafamilia hao katika maisha yao ya kawaida kuamua kujitoa kuingia utume huo.
Alibainisha kwamba kwa njia hiyo Waoblate wanajiimarisha zaidi katika imani na maisha yao ya kiroho kwa njia ya Sala na mafunzo mbalimbali ya kiroho kupitia maisha yao ya Oblate.
Naye Mwenyekiti wa Watawa wa Tatu wa Shirika la Mtakatifu Benedikto Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam,Teodas Mbiro, amewataka waamini wenye nia ya kujiunga katika utume huo, wafuate utaratibu kwa kupatiwa kwa mafundisho ya mwaka mmoja na watapokelewa rasmi.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.