Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

DART yashauriwa kupeleka huduma kwenye Majiji

Waziri Wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Angela Kairuki (katikati) akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) wakati wa ziara ya kutembelea ujenzi wa Barabara ya Mwendokasi kutoka Gerezani Kariakoo hadi Gongolamboto, Dar es Salaam. Waziri Wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Angela Kairuki (katikati) akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) wakati wa ziara ya kutembelea ujenzi wa Barabara ya Mwendokasi kutoka Gerezani Kariakoo hadi Gongolamboto, Dar es Salaam.

Dar es Salaam

Na Israel Mapunda

Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), imeishauri Serikali kutunga Sheria ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dar Rapid Transit Agency: DART), ili kupeleka huduma hiyo katika majiji yote nchini.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Denis Londo alisema hayo wakati wa ziara ya kamati hiyo ya kutembelea na kukagua ujenzi wa barabara ya mabasi ya haraka kutoka Gerezeni Kariakoo hadi Gongolamboto.
Londo alisema kuwa kuna haja kwa Serikali kuandaa maeneo ili kupunguza gharama ya fidia kutokana na miradi mingi ikifanyika na kuwa na gharama kubwa kwa sababu ya ulipaji fidia.
Alisema pia kuwa mitambo ya wakandarasi inapoisha, serikali inatakiwa kuichukua mitambo hiyo na kuendelea kutumia katika miradi mingine, na siyo kuitelekeza au kuiuza kama vyuma chakavu.
Wabunge hao walisema kwamba katika kuweka miundombinu ya miradi ya barabara, kuwe na ushirikiano wa kuandaa na kutenga maeneo mapema yatakayotumika, ili kukwepa kulipa fidia pindi watakapohitaji kuendeleza miji.
Kamati hiyo imesema pia kwamba kuna haja kwa Serikali kuandaa maeneo ili kupunguza gharama ya fidia kutokana na miradi mingi imekuwa ikifanyika na kuwa na gharama kubwa ambayo inachangiwa na ulipaji fidia.
Naye Waziri Wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Angela Kairuki, alisema kuwa uwepo wa DART umesaidia kwa kiasi kikubwa sekta ya usafirishaji, akiahidi kuandaa rasimu ya Sheria Mahsusi ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka itakayosaidia kutatua vikwazo katika utekelezaji wa majukumu yao.
Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa DART, Mhandisi Fanuel Karugendo alisema kuwa kuna maelekezo ya kamati wanayafanyia kazi katika utoaji wa huduma bora za usafiri mijini kote nchini.
Alisema kuwa DART imetimiza miaka 15, hivyo wanaendelea na ujenzi wa miundombinu kwa awamu kwa kila maeneo yaliyoanishwa katika jiji la Dar es Salaam.
Hata hivyo, ni ujenzi wa awamu ya tatu ambao unahusisha barabara ya Nyerere hadi Gongolamboto yenye urefu wa kilomita 23.6 ambao mradi huo unatekelezwa kwa mgawanyo wa mafungu mawili, ambapo kipande cha kwanza kinafanywa na Mkandarasi kampuni ya Synohydro kutoka China, na kipande cha pili ni kwa upande wa majengo ambapo mapitio ya usanifu yako katika hatua za mwisho, na yanafanywa na kampuni ya UNITEC Civil Consultants Ltd, ya Tanzania.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.