Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha
×

Warning

Failed deleting 157-twitter.json

Wanamoyo wahimizwa kufanya Toba

Wanachama wa Shirika la Moyo Mtakatifu wa Yesu, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam wakiwa katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Hija kwa Wanamoyo hao, iliyofanyika katika Kituo cha Hija, Pugu, jimboni humo. (Picha na Mathayo Kijazi) Wanachama wa Shirika la Moyo Mtakatifu wa Yesu, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam wakiwa katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Hija kwa Wanamoyo hao, iliyofanyika katika Kituo cha Hija, Pugu, jimboni humo. (Picha na Mathayo Kijazi)

DAR ES SALAAM

Na Mathayo Kijazi

Waamini na Wanachama wa Shirika la Moyo Mtakatifu wa Yesu, wametakiwa kuwa na moyo wa kutubu wanapokosea, na pia kusamehe pale wanapokosewa, kwani huo ndio usafi wa ndani wa mwanadamu.
Wito huo ulitolewa hivi karibuni na Padri Mary Maximus wa Shirika la Watumishi wa Upendo, wakati akihubiri katika Adhimisho la Misa Katatifu ya Hija kwa Wanachama wa Chama cha Kitume cha Moyo Mtakatifu wa Yesu, iliyofanyika katika Kituo cha Hija, Pugu, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.
“Katika maisha yetu ya kila siku, tujitahidi sana kuwa na moyo wa kutubu pale tunapokosea, na pia tusamehe pale tunapokosewa, kwa sababu huo ndio usafi wa ndani wa mwanadamu,” alisema Padri Maximus.
Alisema pia kuwa Moyo Mtakatifu wa Yesu na Moyo Safi wa Mama Bikira Maria, yote husaidia kuleta upendo katika maisha ya wanadamu, kwa kuwa mioyo hiyo ina huruma kwa Ulimwengu.
Akieleza sababu ya kuadhimisha mioyo hiyo miwili kwa wakati mmoja, Padri Maximus alisema kuwa Moyo Mtakatifu wa Yesu ulichukua upendo kutoka kwa Moyo Safi wa Mama Bikira Maria, hivyo haiwezi kutenganishwa.
Aliwataka Wakristo kuepuka kuwa na chuki katika maisha yao, badala yake waishi katika usafi wa ndani ili waweze kupokea baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Padri Maximus aliongeza kuwa ndoa nyingi huvunjika kutokana na kukosa usafi wa ndani, na uaminifu kutoka kwa wanandoa hao.
Padri huyo aliwasisitiza Wakristo kuepuka kukimbilia kwa waganga wa kienyeji wanapohitaji msaada, bali wamkimbilie Mungu pekee, kwani yeye ndiye anayeweza kuwasaidia.
Aliongeza kusema kuwa hata wanapopokea matusi na changamoto mbalimbali katika maisha yao, wanatakiwa kuyapokea, na kisha kuwa wanyenyekevu, wakiiga mfano wa Mama Bikira Maria, kwani yeye ni mnyenyekevu na asiye na hasira.
Padri Maximus alitumia nafasi hiyo kuwasihi Wanamoyo Mtakatifu wa Yesu kuishi maisha ya huruma na upendo, akisema kuwa huo ni utume wao katika Kanisa.
Alisema kuwa ndani ya Moyo Mtakatifu wa Yesu, kila kitu kinapatikana, hivyo waamini wanatakiwa kuitumia fursa hiyo adhimu kukuza utume wao kupitia chama hicho.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.