Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Serikali kusuka kikosi cha ushindi AFCON

Wachezaji wa timu ya Taifa wakishangilia baada ya kufuzu AFCON kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Mohamed V Septemba 2023. Wachezaji wa timu ya Taifa wakishangilia baada ya kufuzu AFCON kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Mohamed V Septemba 2023.

DAR ES SALAAM

Na Nicolaus Kilowoko

Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imeanza kuandaa mkakati wa kuisuka timu ya Taifa kwa lengo la kufanya vyema katika michezo yake mbalimbali ya kimataifa.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Gerson Msigwa (pichani) aliuzungumzia mwelekeo wa michezo kwa nchi ya Tanzania kwa sasa, huku wakiwa wanaendelea kupata nguvu mara baada ya kupewa nafasi ya kuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Mataifa Afrika, (African Cup of Nations: AFCON).
Alisema kuwa kwa sasa wanaandaa mipango ya kukaa na wadau mbalimbali wa michezo kwa lengo la kuanza mchakato wa kuiandaa timu ya Taifa ili iwe bora zaidia, kwa siku za usoni.
Msigwa alisema kuwa kufanya vizuri kwa timu ambazo zinashiriki Ligi Kuu Tanzania na michuano mbalimbali ya Kimataifa kumesaidia kuwa na timu bora ya Taifa, na hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kupata maendeleo kwenye michezo.
“Mwaka 2027 sisi ndio wenyeji wa michuano hiyo, hivyo hatutakiwi kuwa na timu ambayo haina mwelekeo, bali kuandaa timu ambayo itakuwa na ushindani, ila hata kuchukua hilo kombe lenyewe, inawezekana. Wewe si unaona vijana wanaoshiriki kwenye vilabu mbalimbali vya Ligi wanavyoubonda?” Alisema Msigwa.
Alisema pia kuwa Serikali ya Awamu ya Sita kwa sasa imedhamiria kufanya mapinduzi makubwa kwenye sekta ya michezo, kwani tayari Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ametengeneza muunganiko mkubwa wa viongozi katika maeneo mbalimbali.
Msigwa alidai kuwa mikakati ambayo inaendelea kuwekwa, ni kwa ajili ya kuipa hadhi nchi ya Tanzania katika sekta hiyo ya michezo ili ipate heshima yake.
Msigwa aliapishwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenye hafla fupi iliyofanyika  Septemba 26 mwaka huu, Ikulu, Jijini Dar es Salaam akichukua nafasi ya Said Yakubu ambaye amepewa majukumu mengine.
Miundombinu kuelekea katika fainali hizo imeanza kuwekwa sawa, ambapo Visiwani Zanzibar ukarabati wa uwanja umeanza, huku jijini Arusha ukitarajiwa kujengwa uwanja mpya wa kisasa.
Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam utafanyiwa marekebisho madogo ili kuendana na viwango vya kimataifa.

Rate this item
(0 votes)
Last modified on Thursday, 05 October 2023 09:37

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.